MAKAMU WA RAIS DKT. BILLAL AONGOZA KILELE CHA SIKU YA MAZINGIRA KITAIFA NAMANYERE MKOANI RUKWA - LUKAZA BLOG

All You Want is Here | Chochote Unachohitaji Utakipata Hapa

Breaking

Home Top Ad

Responsive Ads Here

Post Top Ad

Responsive Ads Here

MAKAMU WA RAIS DKT. BILLAL AONGOZA KILELE CHA SIKU YA MAZINGIRA KITAIFA NAMANYERE MKOANI RUKWA

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Mohammed Gharib Billal akihutubia wananchi katika viwanja vya sabasaba Mji mdogo wa Namanyere Mkoani Rukwa katika kuhitimisha siku ya mazingira duniani ambayo kitaifa imefanyika Mkoani Rukwa jana tarehe 05.06.2013. Katika hotuba yake hiyo alisisitizia juu ya uhifadhi wa mazingira kwa kutunza vyanzo vya maji, milima na misitu ya asili, kuhifadhi ardhi na kupanda miti katika maeneo yaliyoathirika na usafi wa mazingira kwa ujumla.
Makamu wa Rais Dkt. Mohammed Gharib Billal akikagua kitalu cha miche ya miti mbalimbali ya mjasriamali ndugu Kidevu (kushoto) katika maonyesho kwenye kilele cha siku ya mazingira kitaifa Mkoani Rukwa katika Mji mdogo wa Namanyere wilayani Nkasi jana tarehe 05.06.2013, Kulia ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais-Mazingira Dkt. Terezya Luoga Huvisa.
Makamu wa Rais Dkt. Mohammed Gharib Billal akisoma moja ya vitabu vya uhifadhi wa mazingira wakati akikagua banda la maonyesho la Ofisi ya Makamu wa Rais Mazingira kwenye kilele cha siku ya mazingira kitaifa Mkoani Rukwa katika Mji mdogo wa Namanyere wilayani Nkasi jana tarehe 05.06.2013, Kulia kwake ni Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Injinia Stella Manyanya na Mkuu wa Mkoa wa Katavi Dkt. Rajab Mtumwa Rutengwe. Kulia ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais-Mazingira Dkt. Terezya Luoga Huvisa.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Mohammed Gharib Billal akimkabidhi kikombe na cheti Ndugu Leonard Kapini Makamu mwenyekiti Halmashauri ya Mji Mpanda kwa Halmashauri hiyo kuwa mshindi wa kwanza kitaifa katika usafi wa Miji nchini. Zawadi nyengine waliyopewa ni Pikipiki moja. Jiji la Nyamagana limekuwa la kwanza kitaifa na Manispaa ya Moshi ikiwa Manispaa ya kwanza kitaifa katika usafi wa Mazingira mwaka huu 2013
Baadhi ya viongozi na wafanyakazi wa Halmashauri ya Mji Mpanda wakifurahia kwa pamoja ushindi kwa halmashauri yao kuwa ya kwanza kitaifa katika usafi wa Miji nchini mwaka 2013. Halmashauri hiyo imezawaidiwa cheti, kikombe na pikipiki moja.
Makamu wa Rais Dkt. Mohammed Gharib Billal akikagua mtambo asilia wa kuzalisha umeme kwa kutumia upepo uliobuniwa na mjasiriamali kutoka Mkoani Rukwa wa kampuni ya Ulaya Hydro and Windmill Technology (Kulia), Katikati ni Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Injinia Stella Manyanya na Kulia ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais-Mazingira Dkt. Terezya Luoga Huvisa.
Makamu wa Rais Dkt. Mohammed Gharib Billal akisalimiana na Katibu Tawala Mkoa wa Rukwa Alhaj Salum Mohammed Chima mara baada ya kuwasili kwa helkopta katika viwanja vya Sabasaba katika Mji mdogo wa Namanyere Wilayani Nkasi kwa ajili kushiriki katika kilele cha siku ya mazingira duniani ambayo kitaifa imefanyika Mkoani Rukwa.
Makamu wa Rais Dkt. Mohammed Gharib Billal akipanda mti wa kumbukumbu katika kampeni ya uhifadhi wa mazingira mbele ya Ofisi ya Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Nkasi jana tarehe 05.06.2013 ikiwa ni kuadhimisha siku ya mazingira duniani ambayo kitaifa imefanyika Mkoani Rukwa.
Makamu wa Rais Dkt. Mohammed Gharib Billal akizindua kwa kuwasha mashine mpya ya maji katika bwawa la maji Mphiri ambalo ni chanzo kikuu cha Maji katika Mji mdogo wa Namanyere Wilayani Nkasijana tarehe 05.06.2013. Serikali imetenga jumla ya Tshs bilioni nne (4) kuendeleza chanzo hicho muhimu ambacho asili yake ni chemchem. 
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais-Mazingira Dkt. Terezya Luoga Huvisa akihutubia wananchi ambapo alikemea uharibifu wa vyanzo vya maji na kuwaasa wanasiasa kutofanya siasa zitakazopelekea kuhatarisha uhai wa vyanzo vya maji kwani umuhimu wa maji hauna mbadala. 
Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Injinia Stella Manyanya akizungumza kuwatambulisha baadhi ya viongozi wakuu waliohudhuria maadhimisho ya siku ya mazingira duniani yaliyofanyika kitaifa Mkoani Rukwa. 
Naibu Waziri wa Afya Dkt. Seif Suleiman Rashid akiwataja washindi mbalimbali wa usafi wa mazingira kitaifa katika ngazi ya majiji, manispaa, miji na wilaya ambao walipewa zawadi mbali mbali. Walioongoza ni Halmashauri ya Jiji la Nyamagana (Majiji), Halmashauri ya Manispaa ya Moshi (Manispaa), Halmashauri ya Mji Mpanda (Miji) na Halmashauri ya Wilaya Njombe (Wilaya). 
Katibu Tawala Mkoa wa Rukwa Alhaj Salum Mohammed Chima akizungumza katika maadhimisho hayo. Kushoto ni Msema Chochote (MC) machachari ambaye pia ni Mkuu wa Wilaya ya Kalambo Mhe. Moshi Chang’a.
MC Machachari ambae ni Mkuu wa Wilaya ya Kalambo Mhe. Moshi Chang’a akisherehesha mambo kwa ufasaha kabisa. Nyuma yake ni kundi la taarab la TOT ambalo limekuwa likinogesha sherehe hizo.
Mkuu wa Wilaya ya Nkasi Mhe. Iddi Hassan Kimanta na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Nkasi Ndugu Galikunga wakijadili jambo katika maadhimisho hayo. Hawa ndio viongozi wakuu wa Wilaya ya Nkasi na wenyeji wa maadhimisho ya siku hiyo ya mazingira kitaifa mwaka huu 2013. 
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais-Mazingira Dkt. Terezya Luoga Huvisa akicheza muziki na kundi la Tanzania One Theatre (TOT) waliokuwepo kutumbuiza katika maadhimisho hayo. TOT wakiongozwa na muimbaji wao mahiri Khadija Kopa “Heshima Pesa Shikamoo Makelele”…
Baadhi ya wafanyakazi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Rukwa wakiwa katika banda  lao la maonesho. (Picha na Hamza Temba – Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Rukwa – rukwareview.blogspot.com)

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)

Post Bottom Ad

Responsive Ads Here

Pages