Msemaji wa Kamati ya Mazishi ya Marehemu Albert Mangwea ambaye pia ni Director kutoka Visual lab Bw Adam Juma akielezea ratiba ya Shughuli nzima ya Mazishi itakavyokuwa mara baada ya zoezi la kutoa heshima za mwisho zitakapomalizika
Baadhi ya Wasanii wa Muziki wa Kizazi Kipya Wa Kwanza Kabisa ni Mkoloni akifuatiwa na Madee ambaye ni wa Tatu kutoka Mbele wakitoa heshima zao za mwisho kwa mwili wa Marehemu Albert Mangwea
Msanii Wa Muziki wa Kizazi Kipya Nasibu Abdul almaarufu kama Diamond akipita kutoa heshima zake za mwisho.
Baadhi ya Wasanii wa Fani mbalimbali pamoja na ndugu,jamaa na marafiki wakipita pembezoni mwa jeneza lililobeba mwili wa Marehemu Albert Mangwea na kutoa heshima za mwisho kwa Marehemu Albert Mangwea leo katika viwanja vya leaders
Msanii wa Muziki Keisha (aliyejifunga kiremba Cheupe) akifuatiwa na Noora wakiwa na nyuso za huzuni wakati wakipita kwaajili ya kutoa heshima zao za mwisho leo katika viwanja vya leaders
Wasanii wa fani ya Maigizo hapa Nchini Mzee Magari (aliyeshika Koti jeusi) akifuatiwa na Msanii Natasha Pamoja na Monalisa wakipita kwaajili ya Kutoa Heshima zao Za mwisho kwa Marehemu Albert Mangwea leo katika Viwanja vya leaders
Baadhi ya Ndugu, Jamaa na Marafiki wakitoa Heshima za Mwisho
Jeneza
lenye Mwili wa Marehemu Albert Mangwea likiwa juu ya meza tayari kwa
Wakazi wa Jiji la Dar Kuanza kutoa Heshima Zao za Mwisho katika Viwanja
Vya Leaders leo.
Mwakilishi kutoka Wizara ya Habari, utamaduni na Michezo Bi Lilian Bereko akitoa Salamu za Rambirambi kutoka Wizara ya Habari, Utamaduni na Michezo leo katika viwanja vya leaders kabla ya Wakazi wa Jiji la Dar hawajaanza kutoa heshima zao za mwisho
Mmoja kati ya watu wa karibu wa Marehemu Albert Mangwea ambaye pia ni msanii wa muziki wa Kizazi kipya kutoka Katika Kundi aliloanzisha Marehemu Albert Mangwea Mez B akitoa historia fupi ya Kundi la Chamber Squade katika viwanja vya leaders leo
Baadhi ya wakazi wa jiji la Dar pamoja na vitongoji vyake wakiwa wamekaa tayari kwa kusubiria shughuli ya kutoa heshima za mwisho kwa mwili wa marehemu Albert Mangwea leo katika viwanja vya leaders
Baadhi ya Wakazi wa Jiji la Dar wakiwa na Nyuso Za Huzuni wakati wa kuaga mwili wa Marehemu Albert Mangwea leo katika Viwanja vya Leaders
Baadhi ya wakazi wa Jiji la Dar wakiwa kwenye foleni ya kwenda kutoa heshima zao za mwisho pamoja na kuuaga mwili wa Marehemu Albert Mangwea leo katika Viwanja Vya Leaders
Askari Polisi wakijaribu kuweka mambo sawa ili kusudi wakazi wa Jiji la Dar pamoja na vitongoji vyake kuweza kuingia kwaajili ya kutoa heshima zao kwa utaratibu mzuri na kuepusha vurugu
Baadhi ya wakazi wa jiji la Dar wakiwa wanatoka kutoa heshima zao za Mwisho
ENDELEA KUWA NASI PICHA ZAIDI ZINAKUJIA MUDA SI MREFU
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)