JAAZI KUNOGESHA REDDS MISS ARUSHA - LUKAZA BLOG

All You Want is Here | Chochote Unachohitaji Utakipata Hapa

Breaking

Home Top Ad

Responsive Ads Here

Post Top Ad

Responsive Ads Here

JAAZI KUNOGESHA REDDS MISS ARUSHA

Na Woinde Shizza,Arusha

Jahazi morden tarabu ikiwa chini wa muimbaji mashuhuri Mzee Yusuphy inatarajia kuinogesha usiku wa kumsaka mlimbwende wa mkoa wa Arusha (Redds Miss Arusha) inatarajiwa kufanyika June nane mwaka huu katika ukumbi wa triple A uliopo jijini apa.


Akizungumza na waandishi wa habari muandaaji wa shindano hilo Phidesia Mwakatalima alisema kuwa shindano hilo litafanyika usiku wa jumamosi june nane katika uwanja wa ukumbi wa Triple A  uliopo ndani ya jiji la Arusha.


Alisema kuwa jumla ya walibwende kumi na tano 15 kutoka katika vitongoji vitatu vya jiji la Arusha ambapo alivitaja kuwa ni pamoja na kitongoji cha Njiro,Arusha mjini(Arusha city cetre)pamoja na kitongoji cha Monduli.


Alibainisha kuwa mpaka sasa warembo wameshaingia kambini wameanza kujifua kwa ajili ya shindano hilo huku akibainisha kuwa kwa mwaka huu lazima mrembo wa Tanzania (Redds Miss Tanzania )atokee mkoa wa Arusha


Alisema kuwa zawadi mbalimbali zitatolewa ikiwemo kuwasomesha warembo katika vyuo mbalimbali lungha ya kiswahili ,kingereza pamoja na kifaransa.


kwa upande wa wathamini waliothamini shindano hili walisema kuwa ni pamoja na perfect choice super markety,libeneke la kaskazini blog,trile A fm,Radio 5 fm,sunrise Fm,Mambo Jambo Fm,Alayance france,Geo Securty,Cassaranda wear,Meru Spring Water Pamoja na Otakef

Motel.

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)

Post Bottom Ad

Responsive Ads Here

Pages