JIJI LA TEXAS NCHINI MAREKANI LAKUMBWA NA MLIPUKO, WATU ZAIDI YA 100 WAHOFIWA KUPOTEZA MAISHA - LUKAZA BLOG

All You Want is Here | Chochote Unachohitaji Utakipata Hapa

Breaking

Home Top Ad

Responsive Ads Here

Post Top Ad

Responsive Ads Here

JIJI LA TEXAS NCHINI MAREKANI LAKUMBWA NA MLIPUKO, WATU ZAIDI YA 100 WAHOFIWA KUPOTEZA MAISHA

 
Mlipuko umetokea katika kiwanda cha kutengeza mbolea karibu na Waco, katika jimbo la Texas nchini Marekani huku idadi kubwa ya watu wakijeruhiwa na wengine kukwama ndani ya kiwanda hicho 
 
Moshi mkubwa uliokena ukipanda juu kutoka katika eneo la mlipuko. Wazima moto na magari ya Ambulance pamoja na helikopta sita zilionekana zikiwasaidia majeruhi.
Wazaima moto hapa wakipambana na moto huo karibu na kiwanda hicho. Majengo kadhaa yaliharibiwa vibaya mengina yakiwa katika maeneo jirani.
Wazee waliokuwa katika makao jirani ya kuwatunza wazee, walihamishwa mara moja. Kulikuwa na ripoti kuwa wazima moto walikuwa wanajaribu kuzima moto wakati mlipuko huo ulipotokea. 
 
 Uharibifu mkubwa ulitokea kwa makao ya kuwahifadhi wazee. Mlipuko ulitokea nyakati za usiku wa kuamkia leo

Zaidi ya watu 100 wamejeruhiwa katika mulipuko uliotokea kwenye kiwanda cha mbolea kilichoko Kaskazini Magharibi mwa eneo la Waco, jimbo la Texas. Wengi wamekwama ndani ya majengo yanayendelea kuteketea kufuatia mulipuko huo.
 
Meya wa Mji kulitokea mulipuko huo, Tummy Muska ameelezea kutokea moto mkubwa uliolipuka sawa na bomu. Mulipuko huo umeharibu majengo ya kiwanda hicho, makaazi ya karibu kikiwemo kituo kimoja cha afya.
Wazima moto, magari ya kubebea wagonjwa na helikopta sita zimetolewa kushughulikia majeruhi na kutuliza hali ya sasa.
 
Majengo kadhaa yameendelea kuteketea karibu na kiwanda hicho cha mbolea.Taarifa ambazo hazijathibitishwa zinasema zinasea kuna watu waliopoteza maisha.
 
Dean Wilson wa idara ya usalama ya Texas amesema nyumba 75 karibu na jengo hilo ziliharibiwa kabisa.
 
Amesema kufikia sasa hawezi kuthibitisha vifo vyovyote. Watu 38 wameripotiwa kua katika hali mahututi. Makundi ya wokozi yameanza kufika nyumba hadi nyingine kuwaokoa majeruhi na kutoa huduma ya kwanza.
 
Kituo cha Dharura kimewekwa kwenye uwanja wa mpira ulioko karibu.Gavana wa Texas amesema afisi yake imetoa raslimali zake kusaidia katika juhudi za wokozi.


  Chanzo: BBC SWAHILI

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)

Post Bottom Ad

Responsive Ads Here

Pages