TAJI LA MISS EAST AFRICA LABAKI TANZANIA HUKU MREMBO JOCELYNE MARO AKINYAKUA TAJI HILO - LUKAZA BLOG

All You Want is Here | Chochote Unachohitaji Utakipata Hapa

Breaking

Home Top Ad

Responsive Ads Here

Post Top Ad

Responsive Ads Here

TAJI LA MISS EAST AFRICA LABAKI TANZANIA HUKU MREMBO JOCELYNE MARO AKINYAKUA TAJI HILO

 Mrembo wa Afrika Mashariki 2012  (Tanzania), Jocelyne Maro (katikati) akiwa na mshindi wa pili (Uganda),Ayisha Nagudi pamoja na Mshindi wa tatu (Burundi),Ariella Kwizera mara baada ya kupatikana kwa washindi hao katika Shindano lililofanyika kwenye Ukumbi wa Mlimani City,Jijini Dar es Salaam usiku wa kuamkia leo.
Mshindi wa taji la Afrika Mashariki Kutoka Tanzania Jocelyne Maro akiwapungia mkono watazamaji mara baada ya kuvalishwa taji la Afrika Mashariki usiku wa Kuamkia leo Ndani ya Ukumbi wa Mlimani City
Mrembo wa Afrika Mashariki 2012  (Tanzania), Jocelyne Maro akipongezwa na washiriki wenzie walioingia kwenye hatua ya tano mara baada ya kutangazwa kuwa ndiye Mrembo wa Afrika Mashariki Kwa Mwaka 2012/2013 usiku wa kuamkia leo
Hii ndio tano bora iliyoingia kwenye Kinyang'anyiro Na Hatimaye Kumfanya Mtanzania Kuibuka Mshindi
Warembo wakipita Jukwaa Kwa Mikato Tofauti tofauti
Mshereheshaji Gaetano Kutoka Uganda akiendelea na Majukumu hapo
Eti hawa Wanaitwa Vijana wa Tigo Kisa staili yao ya Kuimba inafanana na tangazo la tigo wabongo bana....The Voice Wonder hao wakifunika mbaya.
 Burudani Safi Kutoka Kwa Mad Ice
Bloggers na Waandishi wa habari wakiendelea na kazi ya kurusha matukio live
Hapa mmiliki wa Lukaza Blog (Wa Pili Kushoto) niliponaswa na kamera wakati nikiwajibika Haswa
 Wadau mbali mbali walifikika katika Ukumbi wa Mlimani City jijini Dar kushuhudia Mrembo wa Afrika Mashariki anavyopatikana.
 Mkurugenzi wa Rena Event Bw. Rena Calist wa pili kutoka kulia akifuatilia kwa karibu jinsi shindano lilivyokuwa likiendeshwa kulia ni mmoja wa maofisa wa Miss East Afrca John Momadi

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)

Post Bottom Ad

Responsive Ads Here

Pages