WASHIRIKI WA MPANGO WA MAMA SHUJAA WA CHAKULA UNAODHAMINIWA NA NMB WAINGIA KATIKA KIJIJI CHA MAISHA PLUS - LUKAZA BLOG

All You Want is Here | Chochote Unachohitaji Utakipata Hapa

Breaking

Home Top Ad

Responsive Ads Here

Post Top Ad

Responsive Ads Here

WASHIRIKI WA MPANGO WA MAMA SHUJAA WA CHAKULA UNAODHAMINIWA NA NMB WAINGIA KATIKA KIJIJI CHA MAISHA PLUS

Mgeni rasmi katika uzinduzi wa kijiji cha Maisha Plus Naibu Waziri wa Jinsia, Wanawake na Watoto Mhe. Ummy Mwalim  akitoa hotuba wakati wa uzinduzi wa shindano hilo kwenye kijiji cha Maisha Plus. Washiriki wa mpango wa mama shujaaa wa chakula unaodhaminiwa na benki ya NMB hatimaye  wameingia katika kijiji cha Maisha Plus. NMB inaamini udhamini huo ni sahihi kutokana na kuwa utakuza kilimo na kuwasaidia wakulima wadogo katika maisha, mapambano dhidi ya njaa,umasikini na uhaba wa ajira miongoni mwa wanawake.

Vilevile, NMB kupitia mpango wa NMB Financial Fitness unaolenga kuongeza uelewa wa matumizi mazuri ya fedha itapata fursa ya kuwaelimisha washiriki kuhusu huduma za kifedha, uwekaji akiba, kupanga matumizi, matumizi mazuri ya kifedha na mengine mengi.
Naibu Waziri wa Jinsia, Wanawake na Watoto Mhe. Ummy Mwalim (kushoto) na Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Kimataifa Oxfam Bi. Monica Gorman wakifurahia kinywaji cha dafu wakati wa uzinduzi huo.
Mkurugenzi wa Shindano la Maisha Plus Bw. Masoud A. Kipanya (kushoto) akijadili jambo na Mkuu wa Masoko na Mawasiliano wa NMB, Bw. Imani Kajula (kati) pamoja na wageni waalikwa katika uzinduzi huo.
Washiriki wa shindano la Maisha plus wakifuatilia uzunduzi huo huku wakiburudika kwa kinywaji cha dafu.
Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Kimataifa la Oxfam Bi. Monica Gorman (kushoto) akiteta jambo na Naibu Waziri wa Jinsia, Wanawake na Watoto Mhe. Ummy Mwalim (kushoto) pamoja na Mkuu wa Masoko na Mawasiliano wa NMB, Bw. Imani Kajula

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)

Post Bottom Ad

Responsive Ads Here

Pages