MATUKIO YA MGOMO WA WALIMU JANA WANAFUNZI WAANDAMANA KUWAPINGA - LUKAZA BLOG

All You Want is Here | Chochote Unachohitaji Utakipata Hapa

Breaking

Home Top Ad

Responsive Ads Here

Post Top Ad

Responsive Ads Here

MATUKIO YA MGOMO WA WALIMU JANA WANAFUNZI WAANDAMANA KUWAPINGA

 Baadhi ya wanafunzi wa shule za Msingi za jijini Dar es Salaam, Morogoro na Singida, wakiandamana leo asubuhi kupinga hatua ya walimu kugoma kuingia madarasani kufundisha jambo ambalo wanafunzi hao wamelielezea kuwa ni kunyimwa haki zaoza msingi kuwakosesha masomo, ambapo nao wamepanga kutinga Mahakamani kuwafungulia kesi walimu wao kutokana na kwamba madai wanayoidai Serikali wao hayawahusu na hawahusiki kwa mamna yeyote ile, alisikika mmoja wa viongozi wa wanafunzi hao aliyejitambulisha kwa jina la Shaban Mudunda.
 DAR:- Wananfunzi wa Shule ya Msingi Mbezi ya Jijini Dar es Salaam, nao hawakuwa nyuma katika kudai haki yao ambapo nao walifikisha ujumbe kwa njia hii ya Bango, wakiwa pembezoni mwa barabara Morogoro leo asubuhi.
 Nako Mkoani Singida wanafunzi walijitokeza kwa wingi katika mitaa ya mji huo huku wakiimba na wakiwa na baadhi ya Mabango yenye ujumbe kuhusu tukio hilo la kugoma kwa walimu.
 Hawa ni Wanafunzi wa shule za msingi za Ipembe, Nyerere, Unyankindi na Singidani ktk Manispaa Singida, wakiwa nje ya Ofisi za Mkuu wa mkoa huo leo asubuhi, ili kumfikishia ujumbe baada ya walimu wao kugoma.
Wakati walimu wakigoma kuingia madarasani leo asubuhi na wanafunzi wengine kushika mabango na kuandama ili kufikisha ujumbe wa kudai hazi zao, ilikuwa ni tofauti kwa wanafunzi hawa wa Shule ya Msingi Yeta, ambao wao waliamua kuwaonyesha walimu wao kuwa hata wao wanaweza ambao wanafunzi wa Darasa la Saba waliamua kujitolea na kutinga madarasa ya chini na kushusha Nondoz kwa wadogo zao. 

Na katika Shule ya Msingi Lugalo, leo baada ya walimu kugoma wanafunzi wa shule hiyo, walifundishwa na Ma MP pamoja na wanafunzi wa Darasa la saba walifanya kama ambavyo wamefanya wanafunzi wa Yeta amapo wao pia wamejitolea kuwafundisha wadogo zao wa madarasa ya chini.
********************************************

Na: Elisante John Singida.
MGOMO Uliondaliwa Chama cha walimu CWT nchini, umeleta madhara katika Manispaa Singida, baada ya wanafunzi wa shule za msingi kuandamana hadi ofisi za Mkuu wa Mkoa leo asubuhi.

Kwenye maandamano hayo, watoto wa shule za msingi Nyerere, Singidani, Ipembe na Unyankindi, waliamua kutembea umbali wa kilomita tatu hadi ofisi za Mkuu wa Mkoa, wakiwa na mabango yenye ujumbe mbalimbali huku barabarani wakiimba '‘tunataka haki zetu, walimu wamegoma, tunataka haki zetu'’.

Baada ya askari polisi kubaini usalama wa watoto hao upo hatarini, waliingilia kati na kuongoza maandamano hayo hadi ofisi za Mkuu wa Mkoa kwa amani.

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)

Post Bottom Ad

Responsive Ads Here

Pages