Epiq Bongo Star Search yasaka washiriki Club Vybes, jijini Mbeya leo na kesho - LUKAZA BLOG

All You Want is Here | Chochote Unachohitaji Utakipata Hapa

Breaking

Home Top Ad

Responsive Ads Here

Post Top Ad

Responsive Ads Here

Epiq Bongo Star Search yasaka washiriki Club Vybes, jijini Mbeya leo na kesho

Meneja Mauzo wa Zantel mkoani Mbeya, Agrey Mwakilema  nimiongoni mwa watu kibao waliojitokeza kuchangia damu, zoezi ambalo limepokelewa vyema na vijana waliojitokeza katika usaili huo siku ya kwanza hapa Club Vybes.
 Majaji sasa waliingia kazini na hapa wapo makini kumsikiliza mmoja wa washiriki katika usaili huo. Kutoka kushoto ni Master J, Madam Ritha na Salama Jabir. Kazi ilikuwa ngumu maana zaidi ya vijana 600 leo tu walijitokeza sijui kesho itakuaje.
 Vijana wakiwa nje wakisubiri kuingia katika mchujo.
 Huyu kwa leo amevunja rekodi ya Mkoa wa Mbeya ni mshiriki mdogo kuliko wote aliyeingia katika usaili kutoMbeya na anaenda kwa jina la GOODLUCK BROWN. Akina Dogo Janja kibao mwaka huu huenda wakapatikana kama hawa wa Mbeya
Majaji wa EPIQ BSS wakiwa wamesimama kimya kwa dakika mbili ili kutoa heshima kwa watu waliopoteza maisha katika ajali ya Boti ya MV Skagit iliyozama juzi huko Zanzibar kabla ya kuazan kwa usaili wa vijana watakao shiriki shindano hilo kutoka Mkoani Mbeya ambapo zoezi linafanyika kwa siku mbili Julai 21-22, 2012 katika ukumbi wa CLUB VYBES mjini Mbeya. Majaji hao kutoka kushoto ni  Salama Jabir, Madam Ritha,  Masta J na Meneja Mawasilino wa Kampuni ya simu za mkononi ya Zantel, Awaichi Mawala.
 Vijana kibao wa mjini Mbeya wamejitokeza kuwania nafasi ya kuwakilisha mkoa huo katika shindano la EPIQ BSS mjini Mbeya na hapa ni vijana waliofika Club Vybes katika usaili wakibandika namba zao.
 Baadhi ya washiriki waliojitokeza katika usaili huo wakiwasikiliza maelekezo kutoka kwa wasimamizi kabla ya kwenda mbele ya majaji.
 Vijana wakijipanga mistari kwenda kupokea namba na huku wengine wakiondoka baada ya kupata namba zao na wanasubiri kwenda kushuka mistari yao kwa majaji.Picha Father Kidevu Blog

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)

Post Bottom Ad

Responsive Ads Here

Pages