Simba na Yanga zakabidhiwa vifaa - LUKAZA BLOG

All You Want is Here | Chochote Unachohitaji Utakipata Hapa

Habari Mpya

Simba na Yanga zakabidhiwa vifaa

Meneja wa Kinywaji cha Kilimanjaro Bw. George Kavishe akizungumza na waandishi wa habari, katika mkutano uliofanyika katika ofisi za Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini Tanzania TFF wakati kampuni ya bia ya TBL ilipokabidhi vifaa vya michezo kwa timu za Simba na Yanga, tayari kwa kuanza mzunguko wa pili wa Ligi Kuu ya Vodacom inayotarajiwa kuanza Jumamosi Januari 20 2012.
Kutoka kulia ni Katibu Mkuu wa TFF Angetile Osiah, Steven Kilinde Mkurugenzi wa Mahusiano TBL, George Kavishe Meneja wa kinywaji cha Kilimanjaro, Evodius Mtawala Katibu Mkuu wa Simba na Boniface Wambura Msemaji wa TFF wakionyesha vifaa vilivyokabidhiwa ka timu ya Simba.
Mkurugenzi wa Mahusiano wa kampuni ya bia ya Serengeti Steven Kilinde akikabidhi jezi kwa Katibu Mkuu wa timu ya Yanga Selestine Mwesigwa katika hafla ya makabidhiano iliyofanyika katika ofisi za Shirikisho la mpira wa miguu nchini Tanzania leo katikati ni Meneja wa Kinywaji cha Kilimanjaro Bw. George Kavishe na kushoto ni Katibu Mkuu wa TFF Angetile Osiah. Kutoka kushoto ni Mkurugenzi wa Mahusiano wa kampuni ya bia ya Serengeti Steven Kilinde, Meneja wa Kinywaji cha Kilimanjaro Bw. George Kavishe, Katibu Mkuu wa timu ya Yanga Selestine Mwesigwa na kushoto ni Katibu Mkuu wa TFF Angetile Osiah wakionyesha vifaa vilivyokabidhiwa kwa timu ya Yanga katika hafla ya makabidhiano iliyofanyika katika ofisi za Shirikisho la mpira wa miguu nchini Tanzania leo.
Viongozi wa Yanga na Simba pamoja na TBL wakiwa katika picha ya pamoja baada ya makabidhiano ya vifaa vya michezo kwa timu ya Simba na Yanga.

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)


Pages